Tumempoteza kiongozi hodari, poleni sana-Makamu wa Rais Dkt.Mpango

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wamefika Salasala jijini Dar es salaam nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema ili kutoa pole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema wakati alipofika Nyumbani kwa Marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Agosti 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Bi. Doreen Kimbi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema wakati alipofika kutoa pole nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam.

Sambamba na kuifariji familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha kiongozi huyo aliyefariki tarehe 21 Agosti 2022 katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Akiwa nyumbani hapo, Makamu wa Rais amewapa pole wana familia na kuwaomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwafariji wanafamilia, viongozi na wanachama wa TLP alipofika msibani nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema eneo la Salasala jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiongoza sala ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema walipofika msibani nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema, marehemu Mrema alikuwa ni kiongozi mkweli na mzalendo kwa taifa ambapo wakati wote alitetea maslahi ya nchi.

Amesema, taifa limepoteza kiongozi aliyetumikia vizuri nafasi zote alizowahi kuongoza katika uhai wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news