Waziri Simbachawene: Mzee Kusila amefanya mambo mengi ya kuigwa

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amesema Mzee William Kusila alipenda kuona viongozi wanazingatia miiko, na kuishi kwa kuwa mfano mwema kwa jamii.
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Mzee William Kusila katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwake Kijiji cha Mtitaa-Bahi mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipokuwa akitoa salamu za serikali katika ibada ya mazishi ya Mzee Williamu Jonathan Kusila aliyezaliwa mwaka 28/02/1944 na kufariki 21/08/2022, iliyofanyika nyumba kwake kata ya Mtitaa-Bahi Dodoma tarehe 26, Agosti 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Mzee William Kusila.

“Mzee Kusila ni kipimo cha mtu muadilifu; mtu mwenye Upendo, na mtu aliyefanya mambo mengi mazuri ambayo tunapaswa kuyaiga na kuyaenzi.”
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee William Kusila.

"Tumepoteza kiongozi wa kisiasa aliyeshika nafasi mbalimbali za umma na kutimiza majukumu yake ipasavyo, ni mtu aliyepinga na kukataa rushwa,"alisema Waziri.

Aidha ametoa rai kwa Watoto wa Mzee Kusila kuzidi kushirikiana na kushikamana ili kutunza jina na heshima ya baba.

“Amefafanua watu hawazaliwi sawa, mtatofautiana kwa uwezo wa elimu, uwezo wa kipato na mambo mengine lakini wote ni Watoto wa mzee Kusila ni lazima mtengeneze mamlaka itakayosaidia kuwaongoza kama familia,”amesema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Mzee William Kusila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Saba wa Dodoma kati ya Mwaka (1993-19995) alikuwa Mbunge wa jimbo la Bahi na katika vipindi tofauti amekuwa waziri wa kilimo, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi na amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma.

“Alifanya kazi kwa upendo Mkubwa; aliokuwa nao kwa wananchi wa Dodoma, Baba yetu aliongoza kwa Vitendo na sio kwa kuagiza, kama alisema limeni nayeye alikuwa analima”
Mhe. Adamu Kimbisa akisaini Kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee William Kusila. (Picha na OWM).

Naye Mbunge Mstaafu wa jimbo la Chilowa Mhe. Hezekiah Chibulunje akitoa salamu za rambirambi amesema anamkumbuka mzee Kusila kwa jitihada zake za kuondoa Njaa Dodoma na kuhakikisha tunapanda mazao yanayostahimili ukame.

“Alikuwa na uchungu sana katika kuondoa njaa na vile vile katika suala la zima la kusimamia elimu, nimefanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa sana bila nongwa,”amesema

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news