Wizara ya Mambo ya Nje yawaunganisha waandishi wa habari na TICAD 8 Tunis

NA GODFREY NNKO

WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewatangazia waandishi wa habari wote watakaopenda kushiriki katika Mkutano wa Nane wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Afrika (The Eighth Tokyo International Conference on African Development-TICAD 8) utakaofanyika tarehe 27 na 28 Agosti 2022 jijini Tunis nchini Tunisia, kujiandikisha kwa njia ya mtandao.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo Agosti 9, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya leo, mwandishi au waandishi ambao wapo tayari kushiriki katika mkutano huo wajiandikishe kupitia https://www.ticad8.tn kabla ya terehe 14 Agosti 2022.

"Wanahabari watakaoshiriki katika mkutano huo watalazimika kujigharamia usafiri, malazi na masuala mengine katika kutimiza majukumu yao,"imeeleza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments