NBC Lugalo Patron Trophy kufanyika Agosti 27

NA DIRAMAKINI

SHINDANO la Mchezo wa Golf la kumuenzi aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo la NBC Lugalo Patron Trophy linatarajiwa kufanyika Agosti 27,2022 katika viwanja vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) Lugalo jijini Dar es Salam.

Akizungumzia ujio wa shindano hilo Mwenyekiti wa klabu Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luongo amesema,pia lengo la shindano hilo ni kumkaribisha mlezi mpya wa klabu ambaye ni mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Benki ya NBC ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Wateja binafsi na Wateja Wadogo, Ellibariki Masuke ameishukuru Klabu ya Lugalo Gofu kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo na amewaomba wadau na Watanzania wajitokeze kwa wingi katika shindano hilo.

Benki ya NBC imekabidhi vifaa vya Mchezo wa Gofu ambavyo vitatumika katika shindano hilo,NBC Lugalo Patron Trophy linarotarajiwa kufanyika mwezi huu ambapo mgeni rasmi katika ufungaji wa shindano hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa.


Pia amesema, lengo ni kumuaga aliyekua Mlezi wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Gofu, Jenerali mstaafu Venance Mabeyo na kumkaribisha rasmi Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news