Wizara yabuni njia bora kutoa huduma ya maji safi na salama Same

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea eneo hilo na kushuhudia Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani wakiendelea na uchimbaji wa visima viwili. Mheshimiwa Mahundi amesema utekelezaji huo ni katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi karibu na makazi yao.
Mhe. Mahundi amesisitiza kuwa, Wizara ya Maji inaendelea na ukamilishaji wa mradi mkubwa wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe ambao utawezesha upatikanaji wa maji ya kutosha katika Miji ya Same, Mwanga hadi Korogwe.

Amewataka wananchi wa Same kuendelea kuiamini serikali kwani Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua kama mama ambaye anatambua changamoto wanayo kutana nayo wakina mama wenzake hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Pangani Segule Segule amesema visima hivyo vinavyochimbwa vitakuwa na urefu wa zaidi ya mita 250 kila kimoja, lengo ni kuhakikisha maji yanayopatikana yanatosheleza mahitaji ya wananchi walio wengi.

Post a Comment

0 Comments