DKT.JINGU AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA TAIFA YA SENSA YA WATU NA MAKAZI

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu ameongoza kikao cha 8 cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilicholenga kupokea taarifa ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 iliyofanyika tarehe 23 Agosti, 2022 pamoja na kujadili Rasimu ya Mwongozo wa Matumizi ya Takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akizungumza wakati wa kufungua kikao cha 8 cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilichofanyika tarehe 27 Septemba, 2022 kilicholenga kupokea na kujadili Taarifa ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi 2022.Kikao kilifanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere Interational Covention Centre Jijini Dar es Salaam (JNICC).

Kikao hicho kilifanyika tarehe 27 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Julius Nyerere Interational Covention Centre Jijini Dar es Salaam (JNICC).
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa ambaye ni Katibu wa Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi akiwasilisha taarifa ya masuala ya Sensa ya Watu na Makazi wakati wa kikao cha 8 cha Kamati hiyo kilichofanyika tarehe 27 Septemba, 2022 JijiniDar es Salaam.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati wa kikao cha 8 cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilichofanyika tarehe 27 Septemba, 2022 Dar es Salaam.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Zanzibar Mhe. Balozi Mohamed Haji Hamza akieleza na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya sensa wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean. Ndumbaro akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Bw. Seif Shaaban Mwinyi akiuliza swali wakati wa kikao cha 8 cha Kamati hiyo kilichofanyika tarehe 27 Septemba, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi wakifuatilia kikao hicho.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja akiwasilisha Rasimu ya Mwongozo wa Matumizi ya Takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Jukumu kubwa la Kamati hiyo ni kuishauri Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa inayoongozwa na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar namna bora ya utekelezaji wa masuala ya sensa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news