HONGERA KWA SERIKALI, HILI DARAJA LA WAMI:Uelekeo wa Tanga, Moshi Arusha ni safi

NA LWAGA MWAMBANDE

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania inatarajia kuandika historia nyingine hivi karibuni kwa kuzindua daraja jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 ambao linaundwa na barabara za maingilio kilomita 3.8.

Daraja lina upana wa mita 11.85, ambapo kutakuwa na njia mbili za magari za mita nne kwa kila moja, njia mbili za waenda kwa miguu za mita 1.5 kwa kila moja na 0.425 za kingo za pembeni ya daraja (safety barrier) kwa pande zote mbili.

Huu utakuwa mwendelezo wa mafanikio makubwa ambayo yamefikia na Serikali kupitia Sekta ya Ujenzi ambayo kila kona ya nchi imewezesha utekelezaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo madaraja, barabara na mingineyo.

Daraja hilo lililopo mkoani Pwani ambalo ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 90 licha ya kugharamiwa kwa asilimia 10 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia limetoa mamia ya ajira kwa Watanzania tangu ujenzi wake uanze mwaka 2018.

Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anaendelea kusisitiza kuwa, mafanikio ya miradi mingi ya namna hii inatokana na utayari wa Watanzania kulipa kodi zao kwa wakati, hivyo kwa pamoja yafaa kuyashangilia maendeleo haya ambayo yanatokana na kodi zetu, ungana naye hapa chini kujifunza kupitia shairi;
 
1:Daraja jipya la Wami, asili tisina nane,
Kama wewe ni msomi, kwa pamoja tuungane,
Tuseme tusijihami, Serikali tuione,
Haya ni maendeleo, twapaswa kushangilia.

2:Haya ni maendeleo, twapaswa kushangilia,
Na tena ni matokeo, yake Rais Samia,
Aliposhika koleo, kazi hakuachilia,
Uelekeo wa Tanga, Moshi Arusha ni safi.

3:Uelekeo wa Tanga, Moshi Arusha ni safi,
Kama ziara wapanga, barabara mambo safi,
Daraja washalijenga, umeisha ukorofi,
Madaraja nguzo kubwa, ubora wa barabara.

4:Madaraja nguzo kubwa, ubora wa barabara.
Hapo magari makubwa, yakipita ni imara,
Hakuna kuzibwazibwa, upana wake ni bora,
Kukamilisha daraja, ni hatua kubwa sana.

5:Kukamilisha daraja, ni hatua kubwa sana,
Tutoe heko pamoja, hii kazi njema sana,
Ni kodi zetu pamoja, zinafanya ya maana,
Tuzidi unga mkono, juhudi za Serikali.

7:Tuzidi unga mkono, juhudi za Serikali,
Kwa vitendo na maneno, zithibitike kauli,
Ikibidi tuweke wino, msisitizo kamili,
Twaona yanafanyika, barabara zawa bora.

8:Twaona yanafanyika, barabara zawa bora,
Kwingi wanawajibika, inabadilika sura,
Jinsi zinaimarika, uchumi wawa imara,
Kazi tunakabidhiwa, kutunza ziweze dumu.

9:Kazi tunakabidhiwa, kutunza ziweze dumu,
Jinsi zinavyotumiwa, kuzingatia nidhamu,
Hapo zaweza tumiwa, miaka mingi zidumu,
Barabara madaraja, utunzaji ni muhimu.

10:Barabara madaraja, utunzaji ni muhimu,
Asiwepo wa kufuja, vikazidi tugharimu,
Wajibu wetu pamoja, miundombinu idumu,
Hongera kwa Serikali, hili Daraja wa Wami.

Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news