James Mbatia, Angelina Rutairwa watimuliwa NCCR-Mageuzi

NA DIRAMAKINI

MKUTANO Mkuu wa Chama cha NCCR- Mageuzi umemtimua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia.

Pia umemvua uongozi Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,Angelina Rutairwa.

Mkutano huo umetaka viongozi wote waliohusika na ubadhirifu wa mali akiwemo Mbatia kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ni kupitia mkutano unaofanyika leo Septemba 24, 2022 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe 224 kati ya 368 waliopo kwa mujibu wa Katiba ya chama chao.

Wajumbe hao wamefanya hivyo baada ya Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Haji Ambari Hassan kutaja tuhuma saba zinazomkabili Mbatia na tuhuma mbili za Angelina.

Miongoni mwa tuhuma hizo kwa Mbatia ni kuuza mali za chama, ikiwemo mashamba na nyumba katika maeneo mbalimbali.

Ambari amewaambia wajumbe hao kuwa viongozi hao walipelekewa hati ya mashtaka yao na walitakiwa kujibu ndani ya siku 14 kama katiba yao inavyotaka.

Amesema kuwa,hakujibu mshtaka hayo na wala hakufika katika mkutano huo licha ya kualikwa ili aweze kujitetea mbele ya wajumbe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news