Waziri Balozi Mulamula ateta na wawakilishi wa Ufaransa, Rwanda

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na kuzungumza na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Maendeleo,Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Chrysoula Zacharopoulou katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York.
Waziri Mulamula akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Dke Elsie Kanza (wa kwanza kulia) walipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi zao. (Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimuelezea kuhusu zawadi ya picha aliyompa Waziri wa Nchi anayeshughulikia Maendeleo,Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York. (Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo na namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Ufaransa na namna ya kuendeleza sekta za uchukuzi, muindombinu, kilimo, biashara na uwekezaji nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Maendeleo,Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York. (Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

Viongozi hao pia wamejadiliana namna ya kuongeza ujazo wa biashara kati ya Tanzania na Ufaransa na kuihusisha sekta binafsi katika harakati za kuinua uchumi wa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiangalia kitabu cha taarifa alichopatiwa na  Waziri wa Nchi anayeshughulikia Maendeleo,Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York. (Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

Katika tukio jingine Waziri Mulamula amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi hizo.
Waziri Mulamula alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi zao. (Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

Viongozi hao wajadili namna wanavyoweza kushirikiana kupitia sekta ya biashara, uwekezaji na uchukuzi na hivyo kuchangia harakati za ukuzaji wa uchumi wan chi hizo.

Viongozi hao wako jijini New York kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea nchini Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news