Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM yataka maoni, ushauri wa wananchi kuhusu tozo usikilizwe

NA DIRAMAKINI

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa imekutana katika kikao chake maalum Septemba 7, 2022 chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Kupitia kikao hicho ambacho kilikutana ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, kamati hiyo imeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu ushauri na maoni ya wananchi kuhusu tozo.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 8, 2022 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa-Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Shaka amesema, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea, kutafakari na kujadili kwa kina kuhusu hatua za kibajeti zinazoendelea kuchukuliwa kwa lengo la kupata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kasi ili kuwawekea wananchi mazingira mazuri ya kujipatia maendeleo.

“Eneo moja wapo ikiwa ni kupitia tozo ambapo ni ukweli usiopingika kwamba Serikali imeweza kufanya mambo makubwa katika kipindi kifupi kwa mfano ujenzi wa vituo vya afya 234 na shule mpya za sekondari 214 na maeneo mengine kadhaa ambayo yanagusa maisha ya watanzania ya kila siku.

“Hata hivyo, baada ya kutafakari na kujadiliana kwa kina Kamati Kuu imeona umuhimu wa Serikali kusikiliza maoni na ushauri wa wananchi kuhusu utekelezaji wa bajeti hiyo, hususani katika eneo la tozo za miamala ya kielektroniki, iliyoanza kutekelezwa hivi karibuni,"amesema Shaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news