Tisa wajeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori la mahindi kuyagonga magari Arusha

NA DIRAMAKIN

KAMANDA wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP Justine Masejo amethibitisha kutokea wa ajali iliyohusisha magari matatu jana usiku.

Amesema, ajali hiyo imetokea jana usiku majira saa tatu na robo na kuhusisha gari namba T.673 AXB aina ya Scania lori yenye tela namba T.464 AWZ likiwa na shehena ya mahindi ambapo lilikuwa linatokea Arusha kwenda Namanga na kuyagonga magari mengine matatu madogo ikiwemo T167 BRX aina ya Nissan caravan.

Kamanda Masejo amesema, katika ajali hiyo imesababisha majeruhi tisa ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa matibabu zaidi.

Post a Comment

0 Comments