Karatu washtukia mchezo mchafu wa madaktari wanaojaza taarifa za uongo PF3

NA SOPHIA FUNDI

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wamelaani tabia ya baadhi ya madaktari kutojaza fomu za PF3 kwa waliofanyiwa vitendo vya ukatili kwa kupoteza ushahidi.
Wakizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo walisema kuwa, kumekuwa na tabia za baadhi ya madaktari kujaza taarifa za uongo kupoteza ushahidi jambo ambalo limekuwa likileta sintofahamu kwa waliofanyiwa ukatili.

Madiwani hao wameazimia kwa pamoja na kumwagiza mkurugenzi pamoja na timu ya wataalam wa afya wakiwemo ustawi wa jamii kufuatilia kwa karibu madaktari wanaojaza fomu hiyo ya PF3 na kujaza taarifa za uongo kupoteza ushahidi na pale wanapogundulika wachukuliwe hatua za kisheria.

"Haiwezekani kuwanyamazia madaktari hao hata kama ni wa hospitali za binafsi kuendelea kufanya vitendo hivyo , unakuagiza wote hao wako chini yako kwa maana ya halmashauri, hivyo wachukuliwe hatua haraka kukomesha tabia hizo,"alisema Diwani Lucian.
Lucian amewaomba madiwani katika maeneo yao kushirikiana na wataalam kuwahamasisha wananchi kufichua vitendo vya kikatili wanazofanyiwa wananchi hasa wanawake na watoto ikiwemo ubakaji na ulawiti.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmshauri hiyo, Karia Magaro alisema kuwa halmashauri hiyo imejipanga kutdibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya kata.Aliwaomba wananchi kuacha tabia ya kulindana na kuficha taarifa za ukatili, bala yake waripoti kwenye kamati za kudhibiti vitendo vya kikatili kwa wanawake na watoto zilizoko kwenye kila kata na pia kwenye dawati la jinsia ili kukomesha vitendo hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news