Waziri Balozi Mulamula atoa pole kwa familia ya Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) ametoa pole kwa Familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Hassan kilichotokea tarehe 31 Agosti, 2022 katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja, Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipoitembelea familia hiyo kwenye makazi yake Jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news