Koffi Olomide ndani ya Mwanza

NA DIRAMAKINI

MSANII Koffi Olomide maarufu Mopao anatarajiwa kufanya shoo katika ukumbi wa The Breez Complex ulioko Sabasaba barabara ya kuelekea Kiseke jijini Mwanza.
Picha na Getty Images.

Mratibu wa shoo ya Koffi Olomide jijini humo, Bwana Victor amesema msanii huyo anatarajia kufanya shoo yake wiki ijayo.

Amesema kuwa, Koffi Olomide atafika jijini Mwanza akiwa na bendi yake kwa ajili ya kuwapa burudani wakazi wa Mwanza na mikoa jirani.

"Niwaombe sana wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kujitokeza katika tamasha kubwa la msanii wa dansi ili muweze kushuhudia mambo makubwa anayoyafanya kwa upande wa viingilio tutawajulisha hivi karibuni hivyo kaeni mkao wa kula,”amesema.

Kiongozi kutoka The Breez, Nashoni Msafiri amesema, wanatarajia kupokea ugeni mkubwa wa msanii Kofii Olomide ambaye anakuja kutoa burudani kwa mashabiki wake na wapenzi wa muziki dansi.

Post a Comment

0 Comments