LIVE:Maziko ya Malkia Elizabeth II

 

Maziko haya yatafanyika leo Septemba 19, 2022, ikiwa taratibu za kuutazama mwili wa Malkia kwa siku nne mfululizo zimekamilika.

Familia yake, wanasiasa na viongozi wa Dunia watahudhuria maziko haya ambayo itakuwa ni siku ya mapumziko inayofahamika kama Bank Holiday.Malkia atazikwa katika kanisa dogo linalofahamika kama King George VI Memorial Chapel lililopo Windsor nchini Uingereza.
 
Malkia Elizabeth II wa Uingereza ambaye anatajwa kuwa ni kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini humo na kuipitisha Uingereza katika nyakati ngumu na nyepesi katika kipindi chote cha utawala wake wa miaka 70 alifariki Septemba 8, 2022 akiwa na miaka 96.

Kasri ya Buckingham ilitangaza kwamba Malkia alifariki akiwa katika kasri ya Balmoral huko Scotland ambako huwa anapumzika katika majira ya joto. Aidha, kwa sasa mwanae Prince Charles mwenye miaka 73 ndiye mfalme kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments