Wavamizi Hifadhi ya Msitu wa Bondo watakiwa kuondoka

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

WANANCHI waliovamia Hifadhi ya Msitu wa Bondo wametakiwa kuondoka ndani ya hifadhi hiyo ifikapo Desemba 30,2022.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilindi, Mhe. Omar Mohamed Kigua bungeni jijini Dodoma leo Septemba 19,2022.

“Kwa nyakati tofauti hifadhi hii imekuwa ikivamiwa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu zikiwemo kilimo,makazi na kuchungia mifugo,” Mhe. Masanja amefafanua.Amesema Serikali imeweka matangazo ya kuwataka wananchi wote kuondoka ndani ya hifadhi hiyo.

Aidha, amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali misitu nchini.

Hifadhi ya Msitu wa Bondo, ipo katika Kijiji cha Mswaki,Kata ya Msanja wilayani Kilindi mkoani Tanga.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news