Mheshimiwa Alhaj Othman ajumuika na waumini sala ya Ijumaa, maziko ya Mzee Hamad

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman,Septemba 16, 2022 amejumuika na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, huko Masjid Lootah, Msikiti uliopo Kiembesamaki, Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja.
Wakati huo huo Mhe. Othman akiambatana na viongozi mbalimbali wa Kisiasa, Kidini na Kijamii, ameshiriki katika Maziko ya Marehemu Mzee Adallah Saleh Hamad, Kaka wa Ndg. Seif Saleh Hamad, ambaye ni Afisa- Mwandamizi katika Kurugenzi ya Oganaizesheni na Wanachama ya ACT-Wazalendo, Zanzibar.

Marehemu amesaliwa katika Masjid Lootah, Kiembesamaki na kuzikwa huko Makaburi ya Mwanakwerekwe, Wilaya ya Magharibi B, kisiwani Unguja.MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI, Amiin!
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Septemba 16, 2022

Post a Comment

0 Comments