KUSINI HUKO KUCHELE:Namna ya kushiriki, mjadala elimika

NA LWAGA MWAMBANDE

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazokua kwa kasi kiuchumi. Kasi hiyo inachochewa zaidi na utulivu wa kisiasa na kiuchumi, sera nzuri na zinazotabirika pamoja na amani na utulivu.

Aidha,Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa fursa nyingi sana katika sekta zote, ingawa Serikali inaweka kipaumbele katika sekta muhimu kama vile Kilimo, Madini, Utalii, Viwanda, Usindikaji wa Kilimo, Dawa, Majengo na Mifugo na Uvuvi.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria na kujitoa ka nguvu zote kuifungua nchi katika uchumi wa Dunia kupitia kuboresha mazingira ya uwekezaji, uendelezaji wa miundombinu mikubwa ili kuharakisha mtiririko mzuri wa Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Nje na Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Ndani kwa jamii na ustawi wa uchumi wa Watanzania.

Pia, Serikali imekuwa ikifanya mageuzi makubwa ya kisheria na kikanuni katika azma ya kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa maeneo bora ya uwekezaji ndani na nje ya Bara la Afrika.

Ni mageuzi ambayo yanaangazia, marekebisho ambayo yanajumuisha utaratibu wa kodi,michakato ya uwekezaji ya moja kwa moja, kuoanisha taasisi, sheria za ardhi pamoja na kufungua vikwazo vinavyozuia ukuaji wa biashara nchini.

Kwa nini Tanzania? Kwa sababu Tanzania ina rasilimali nyingi za asili ambazo zinatoa fursa mbalimbali za kuwekeza. 

Rasilimali hizo ni pamoja na eneo zuri sana la kijografia, ambalo linafanya nchi sita zisizokuwa karibu na bahari kutegemeabandari za Tanzania kama njia rahisi za kuingizia na kutolea bidhaa zao, ardhi nzuri yenye rutuba, vivutio vingi maarufu vya kitalii, kama vile, mbuga.

Mshairi wa kisasa, Bw.Lwaga Mwambande anasema kuwa,ukitaka kuieleza Tanzania kuhusu mema yaliyomo itakuchukua safari ndefu ambayo inaweza kuwa miaka kadhaa, lakini kwa kuanzia ameona akukumbushe kuwa, kule Kanda ya Kusini ambayo inaundwa na mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kuna fursa nyingi, vyanzo vya malighafi, stadi za aina nyingi, uhakika wa nguvu kazi kwa gharama nafuu, usalama wa mali, watu wachangamfu na rafiki kwa uwekezaji. Ungana naye hapa chini;


1:Kusini huko kuchele, mjadala wafanyika,
Fursa zilizo tele, ziweze kufahamika,
Watu wawekeze kule, nchi iweze inuka,
Mikoa yetu mitatu, yao yanajadilika.
UTAKAVYOSHIRIKI MJADALA SOMA HAPA
 
2:Hapo utaje Mtwara, bandari gesi wafika,
Lindi twajua ni bora, gesi imejisimika,
Ruvuma yauza sera, kilimo imekishika,
Mikoa yetu mitatu, yao yanajadilika.

3:Korosho umesikia, huko imekamilika,
Madini utasikia, mengi pia yachimbika,
Shiriki utasikia, utajiri kianika,
Mikoa yetu mitatu, yao yanajadilika.

4:Sasa hivi si zamani, jinsi kunavyofikika,
Ukitaka baharini, huko vema kwapitika,
Angani barabarani, mikoa yaunganika,
Mikoa yetu mitatu, yao yanajadilika.

5:Namna ya kushiriki, mjadala elimika,
Mwenyewe utie tiki, utakavyowajibika,
Lengo mali twamiliki, yote iweze tumika,
Mikoa yetu mitatu, yao yanajadilika.

Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news