MKURABITA yapongezwa kwa kutoa hati miliki za ardhi za kimila

 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo ameipongeza MKURABITA kwa kuwapatia Hati Miliki za Ardhi za Kimila wananchi wa Kijiji cha Manyemba wilayani Chamwino, na kuelekeza hati zote zinazohusisha familia pindi zinapoandaliwa umiliki wake uwe na majina ya akina mama pia badala ya majina ya akina baba pekee.

Mhe. Chaurembo ametoa maelekezo hayo akiwa katika Kijiji cha Manyemba wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake wilayani Chamwino, iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani humo.

Mhe. Chaurembo amesema, MKURABITA licha ya kutekeleza vizuri wajibu wa kujenga masijala na kuwapatia wananchi wa kijiji hicho hati miliki za ardhi, lakini wanapaswa kuzingatia kuwa hati zote za kifamilia umiliki wake uwe na majina ya akina mama na akina baba kwani wote wana haki sawa katika umiliki wa ardhi.

Post a Comment

0 Comments