MWANZA WAIPA KONGOLE OFISI YA KAMISHNA WA ARDHI MSAIDIZI

NA MWANDISHI WETU

OFISI ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Mwanza imepongezwa na baadhi ya wananchi wa mkoa huo kwa kuweza kusimamia na kutekeleza uanzishwaji kliniki za ardhi kwa kuweka kituo jumuishi katika eneo la Rock City Mall mkoani humo kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za sekta ya ardhi.
Wakizungumza katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza tarehe 12 Septemba 2022 wananchi hao wamesema, utaratibu wa kuwa na kituo jumuishi kinachotoa huduma mbalimbali za sekta ya ardhi ni jambo zuri linalopaswa kuigwa siyo tu na ofisi za ardhi katika mikoa bali hata wizara nyingine kwa kuwa linarahisisha kutatua changamoto za wananchi.
Kupitia kituo hicho wananchi wanapata huduma mbalimbali za sekta ya ardhi sambamba na fursa ya kununua viwanja kupitia mradi wa uuzaji viwanja wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayoongozwa na Mhe. Dkt Angeline Mabula kwa sasa iko katika juhudi kubwa za kuhakikisha ardhi ya Tanzania napangwa, inapimwa na kumilikishwa, inaondoa migogoro ya ardhi sambamba na kuiwezesha serikali kukusanya mapato yatokanayo na kodi ya pango la ardhi.

Post a Comment

0 Comments