TANZIA:Askofu John Ackland Ramadhani afariki

NA GODFREY NNKO

ASKOFU Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, John Ackland Ramadhani amefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mwinjilisti Canon Bethuel Mlula imeeleza kuwa, Baba Askofu Ramadhani amefariki Septemba 12, 2022.

"Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Kanisa la Angilikana Tanzania, Maimbo William Mndolwa kwa masikitiko makubwa, anatangaza kifo cha John Ackland Ramadhani, Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania kilichotokea Septemba 12, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.

"Mhashamu Askofu John Ackland Ramadhani alizaliwa huko Zanzibar mnamo tarehe 1 Agosti, 1932 akiwa mtoto wa Mathew Douglas Ramadhani na Bridget Ann Constance Masoud,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo;

Post a Comment

0 Comments