Padri Mapalala:Mungu utupe moyo wa kutosahau kuwa wafadhili wa wengine, kuwashirikisha mali zetu

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameshauriwa kuwa, wanapokuwa na mali wana wajibu wa kuwashirikisha wengine wenye shida na kwa kufanya hivyo wanatimiza lile neno lisemalo nilikuwa na njaa mkanipa chakula.

Haya yamesemwa na Padri Paul Mapalala katika mahubiri ya misa ya leo Jumapili ya Septemba 25, 2022 katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.

“Tukijikita katika injili, tunaona kuwa Lazaro yalimpata yaliyompata na tajiri yalimpata yaliyompata, sisi binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mwenyezi Mungu, hakuna wa kumdharau mwingine, sote ni watoto wake, ndiyo maana katuumba tofauti tofauti, kinachotakiwa zaidi ni upendo na ukadiri wa kutumia mali za duniani, binadamu hatupaswi kugombana wala kudharauliana.”

Akiendelea kuhubiri Padri Mapalala alisema kuwa kila mmoja ni ndugu wa mwingine na kila mmoja ni kiumbe wa Mungu, binadamu anawajibu wa kutimiza wajibu wake, mwenye nacho na asiye nacho, vyote ni mali za Mungu, umaskini au utajiri usilete makundi katika jamii.

Mahubiri hayo yaliyojikita katika masomo mawili na injili ya Jumapili hii ya maskini Lazaro na tajiri yaliambatana na maombi kadhaa;

“Mali ni msingi wa maisha ya binadamu, utupe moyo wa kutosahau kuwa wafadhili wa wenzetu na kuwa tayari kuwashirikisha wenzetu mali zetu ; Mapambano mengi duniani yanatokana na ugawaji wa mali usio sawa, ufungue macho ya wenye mamlaka na mali ili wasiwe na tamaa ya mali na wasigandamize haki za wanyonge .”

Kwa juma zima katika eneo la Chamwino Ikulu na wakati misa hii hali ya hewa na eneo la hili imeendelea kuwa ya baridi kiasi hasa hasa wakati wa usiku na jua la kali wakati wa mchana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news