15 washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya wafugaji, mifugo 159 yapatikana

NA ABEL PAUL, Tanpol

JESHI la Polisi kupitia kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo nchini limesema linawashikilia watuhumiwa 15 waliohusika katika tukio la mauaji ya wafugaji katika Kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.
Hayo yamesemwa Septemba 24, 2022 na Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji nchini, Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP SIMON PASUA alipofika Kijiji cha Mbatamila wilaya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amebainisha kuwa jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa 15 kwa kosa la mauaji ya vijana wanne wa familia moja.

Ni katika Kijiji cha Mbatamila na kusema kuwa wale wote waliofanya mauaji hayo hawako salama na kuwataka wajisalimishe Jeshi la Polisi.
Aidha, amewataka wakulima na wafugaji kutojichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate misingi ya sheria na taratibu katika kutatua Changamoto zilizopo.

Sambamba na hilo amewapa pole wananchi waliopoteza ndugu zao ambapo Kamanda Pasua amesema, jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wote walio baki ili wafikiahwe katika vyombo sheria kujibu tuhuma zinazowakabili. MIFUGO 159

Pia Kamanda Pasua amesema kuwa, jeshi hilo limefanikiwa kukamata mifugo 159 iliyokuwa imeibiwa katika Kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.
Amesema, jeshi hilo linaendelea kushrikiana na wafugaji na wakulima katika kupambana na uhalifu wowote ule.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wafugaji Nchini, Bi. Prisca Kaponda amesema, wao kama chama cha wafugaji kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi ili kumaliza migogoro ya wakuliama nawafugaji hapa nchini.
Aidha,baadhi ya wahanga wa tukio hilo wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa jitihada walizochukua za kuwakamata watuhumiwa wa matukio ya mauaji na kukamata mifugo iliyokuwa imeibiwa katika Kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma na kuliomba jeshi hilo kuweka nguvu kubwa ili kupata mifugo ambayo haijapatikana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news