Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi wawili.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 21, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Shaheen Fauz Mohammed kuwa Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Shaheen kabla ya uteuzi huu alikuwa Mhasibu Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Juma Amour Mohammed kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Juma, kwa sasa ni mshauri wa taasisi mbalimbali za kibiashara, ambapo uteuzi wa viongozi hao umeanza Septemba 21, 2022.

Post a Comment

0 Comments