Rais Dkt.Mwinyi: Misikiti itoe elimu ya dini kwa vijana nchini

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesisitiza umuhimu wa misikiti kutoa elimu ya dini kwa vijana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi na Mwenyekiti wa Kamati ya Masjid Noorul Qadiriya Kandwi, Sheikh Ali Suleiman Mawele, baada ya ufunguzi wa Masjid hiyo na Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo Septemba 30,2022 katika msikiti huo.(Picha na Ikulu).

Alhaj Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 30,2022 baada ya sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Noorul-Qadiriya Kandwi uliopo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwa, misikiti ina kazi kubwa ikiwemo kujitolea kuwafundisha vijana elimu hiyo ili wapate malezi bora.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Kandwi Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo 30-9-2022, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Masjid Noorul Qadiriya Kandwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu).

Amesema, viongozi wa misikiti wanapaswa kufundisha mambo mema na kukemea kwa nguvu zote matendo mabaya ambayo yanafanywa ndani ya jamii ikiwemo vitendo vya udhalilishaji.

Alhaj Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwa, waumini wa dini ya Kiislamu waache kuoneana aibu na badala yake wakemee vitendo hivyo kwa kupaza sauti bila woga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsalimia Mwananchi wa Kijiji cha Kandwi Wilaya Kaskazini “A” Unguja Bi. Miza Baya Khamis, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Masjid Noorul Qadiriya iliyofanyika leo. (Picha na Ikulu).

Kwa upande wake Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi amesema, ifike mahali misikiti itumike kuwafundisha watoto elimu ya dini hatua ambayo itasaidia kuwaritihisha imani, upendo, umoja na maelewano kati yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news