Rais Putin,Xi Jinping kukutana Samarkand

MOSCOW-Rais wa Urusi, Vladmir Putin na Rais wa China, Xi Jinping wanatarajiwa kukutana wiki ijayo katika mkutano huko Uzbekistan.
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na Rais wa China Xi Jinping.(PICHA NA SPUTNIK/KREMLIN VIA REUTERS).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mmoja wa maafisa wa Serikali ya Urusi ambapo amebainisha kuwa, viongozi hao watakutana katika mkutano wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai (The Shanghai Cooperation Organisation (SCO) unaofanyika katika mji wa Samarkand nchini Uzbekistan tarehe 16 Septemba, 2022.

Aidha,Balozi wa Urusi nchini China, Andrei Denisov aliwaeleza waandishi wa habari kuwa,mkutano mwingine wa viongozi utafanyika katika mkutano wa SCO huko Samarkand nchini Uzbekistan.

"Tunajiandaa kikamilifu kwa hilo,"Balozi Denisov alinukuliwa na Shirika la Habari la Tass la Urusi.

Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO) ni shirika la kisiasa, kiuchumi na kiusalama la Eurasia. 
 
Kwa upande wa wigo wa kijografia na idadi ya watu, ni shirika kubwa zaidi la kikanda duniani, linalochukua takribani asilimia 60 ya eneo la Eurasia, asilimia 40 ya idadi ya watu duniani, na zaidi ya asilimia 30 ya Pato la Taifa.

Post a Comment

0 Comments