Rais Samia atoa kongole ujenzi wa Majaliwa Stadium

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kwa ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Majaliwa.

Rais Samia amesema kuwa, ujenzi wa uwanja huo utakuwa chachu katika kukuza sekta ya michezo nchini.

Ameyasema hayo leo Septemba 11, 2022 alipompigia simu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa uwanja huo, katika halmashuri ya Ruangwa mkoa wa Lindi,

“Nawapongeza pia kwa sherehe nzuri ya kuzindua uwanja wa mpira wa miguu wa Majaliwa, uwanja huo pia utatumika kwa ajili ya mazoezi kwa timu zetu.”

Awali, akizungumza na Wana-Ruangwa Mheshimiwa Majaliwa amewashukuru wananchi hao kwa kuamua kuchangia shilingi 200 katika kila kilo moja ya mazao wanayoyauza ili kufanikisha ujenzi wa uwanja huo.

“Natambua mchakato wa ujenzi wa uwanja huu umetokana na mawazo yenu na matamanio yenu, hivyo mkaamua kutekeleza ili tuwe na uwanja huu. Maamuzi yenu ya kuchangia mlicho nacho yametufikisha hapa. Hongereni sana.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kwa ridhaa ya wakazi wa Ruangwa ambao wameridhia kuendelea kuboresha uwanja huo, msimu ujao wa ligi yatawekwa ili kuwezesha sehemu ya mashabiki kukaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news