TFF yafunguka kuhusu wachezaji wa kigeni

NA DIRAMAKINI

USAJILI wa wachezaji wa kigeni, hasa kwa klabu ambazo timu zao zinacheza mashindano ya kimataifa ulishapitishwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji katika mazingira maalumu ilishughulikia haraka usajili wa wachezaji hao wa kigeni ili wawa
hi usajili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Wachezaji wote wa klabu hizo za Azam, Geita Gold, Simba, na Yanga walishapewa leseni zao kwa ajili ya msimu wa 2022/2023 ambazo pia ndizo zimetumika kuwaombea usajili kwa ajili ya mashindano ya CAF.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12. Hivyo, klabu kutaka au kujaribu kusajili wachezaji zaidi ya idadi hiyo ni kwenda kinyume na kanuni.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news