Vijana walioenda kusoma India wamshukuru Prof.Muhongo

NA FRESHA KINASA

VIJANA sita walioombewa ufadhili wa masomo kupitia Programu ya ICCR Scholarships na Mbunge wa Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo kwenda kusoma nchini India wamemshukuru mbunge huyo kwa kuwatafutia ufadhili huo.

Wamesema juhudi za Prof.Muhongo ambaye licha ya kutingwa na majukumu mengi yakiwemo ya jimboni amekuwa mstari wa mbele kusikiliza,kushirikisha,kutatua na hata kuyapatia ufumbuzi mahitaji ya wananchi kadri inavyowezekana.
Vijana hao wamesema kuwa, wao hawana cha kumlipa Mheshimiwa Prof.Muhongo zaidi ya kumuombea Mungu ampe afya, amzidishie hekima na maarifa.

Wanafunzi hao sita walisoma MSc Applied Geology kwenye maeneo yafuatayo:

*Coal Geology

*Metamorphic Geology

*Mineralogy

*Mineral Processing

Wakati huo huo, Mheshimiwa Prof. Muhongo amewapongeza vijana hao kwa kusoma na kufaulu vizuri huku akiwatakia kila la heri katika maisha yao.Vijana hao wote sita wanafanya kazi kwenye taasisi za Serikali hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments