Wataja athari za tozo zikifutwa zote, watoa angalizo kwa Taifa kiuchumi

NA DIRAMAKINI

LEO Septemba 22, 2022 wadau mbalimbali wameshiriki katika mjadala maalum na muhimu wa Kitaifa ukiangazia juu ya punguzo la tozo na faida zake kwa wananchi.
Mjadala huo ambao umerushwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari umeratibiwa na Watch Tanzania kwa njia ya Mtandao wa Zoom. Katika mjadala huo, washiriki wamenena yafuatayo;

WILLIAM MHOJA, KAMISHINA MSAIDIZI IDARA YA SERA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
"Kuhusu kutoza fedha kwa njia ya benki tulitaka kuweka usawa kwamba makato yasiwe tu kwa watumiaji wa miamala ya simu bali hata wale wanaotumia huduma za kibenki wachangie pia maendeleo ya Taifa.

"Kama tutaamua kuzifuta kabisa hizi tozo basi tutachelewa na kurudi nyuma katika kuhakikisha tunatanua wigo wa maendeleo kwa shughuli zile ambazo tumezikusudia na kuikwamua nchi,"amesema.

DKT.ABDALLAH S. MABODI, NAIBU KATIBU MKUU CCM ZANZIBAR

"Mawazo ya waziri yalikuwa mazuri sana kwamba hizi fedha za tozo zitakazo kusanywa zitakwenda kutoa mahitaji ya msingi ya kimaendeleo kwa watu wa hali ya chini, ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, shule, nyumba za walimu, upatikanaji wa vitendea kazi mashuleni na hospitalini n.k.
"Kamati Kuu ya CCM ilikaa chini na kuitaka Serikali ikae kitako ifikirie namna gani tunaweza kuondoa au kupunguza hizi tozo na hasa kwa sababu yale majanga makubwa ambayo tulikuwa nayo yameanza kupungua, tunaishukuru Serikali kwa kutusikiliza,"amesema.

DKT.HEZRON MAKUNDI, MTAFITI TAALAM ZA MAENDELEO ( USDM)

"Sehemu kubwa ya wajibu wa serikali ni pamoja na kusimamia masuala ya fedha, kwani ina nafasi kubwa sana katika uendeshaji wa dola au Taifa, hii ni pamoja usimamizi wa mapato ya ndani kuhakikisha yanasaidia taifa kusonga mbele.
"Kuna changamoto zinajitokeza mfano kwenye upandaji wa mafuta kutokana na vita, hivyo serikali inapoweka ruzuku kwenye lita moja ya petroli ni katika kuhakikisha kwamba sekta binafsi haziumii sana kutokana na changamoto hizi ambazo ni nje ya uwezo wa ndani,"amesema.

MHE. GOODLUCK NG'INGO, MWANADIPLOMASIA NA MCHAMBUZI MASUALA YA KISIASA

"Sote tunakiliri kwamba Serikali Awamu ya Tano na Sita chini ya Mhe.Rais Samia kupitia fedha za makusanyo imetekeleza miradi mingi sana kwa kipindi kifupi kila mtanzania anajua hilo siyo mijini bali asilimia kubwa miradi hiyo ipo vijijini kwa wahitaji zaidi.
"Zaidi ya wananchi milioni 33 wanafanya miamala ya siku na benki kwa idadi hii ni kubwa sana katika ukusanyaji wa fedha ambazo zitakwenda kutunisha mifuko ya ujenzi wa maendeleo, hivyo kikubwa ni kutoa elimu kwa Watanzania kujua na kuelewa umuhimu wake na faida tunayoipata kulikoni kukimbilia kukopa nje ya nchi,"amesema.

AZIM DEWJI, MFANYABIASHARA

"Kwa sisi wafanyabiashara ongezeko hili la tozo lilikuwa linatupa wakati mgumu hasa kwenye ushindani masokoni, kwa sababu tozo ikiongezeka hasa kwenye mazao bei lazima iwe juu, hii inatufanya wale washindani wetu hasa nje ya nchi wanatuzidi kwa sababu bei yetu ipo juu.
"Rais wetu alikuwa na uwezo wa kukataa kujitolea shillingi bilioni 100 kwa ajili ya ongezeko la bei ya mafuta, lakini kwa sababu Rais wetu ni msikivu na mwenye huruma amekuwa akitoa pesa hiyo kila mwezi ambayo hata kama ingetolewa na tozo isingefika hata nusu yake kupitia tozo hizi,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news