'Watu wanasema Al Hilal wana wachezaji wazuri,kisa kuna mchezaji katoka Asec Mimosas je? Hao Al hilal wanajua pia kuwa Eng.Hersi alitoa mtu pale Asec Mimosas?'


"Kumekuwa na habari mbalimbali kuhusiana na ukubwa na ugumu wa mchezo wetu ujao.

“Watu wanasema Al Hilal wana wachezaji wazuri kisa kuna mchezaji katoka Asec Mimosas je? Hao Al hilal wanajua pia kuwa Eng Hersi alitoa mtu pale Asec Mimosas...?
"Wanasema kuna mchezaji katoka As Vita Club na wao je? Wanajua kuwa Yanga SC walimsajili mfungaji bora wao na yupo Yanga kwa sasa.
 
"Wanasema wana mchezaji kutoka Senegal je jiulize wanajua na sisi tuna mchezaji kutoka Burundi ambaye kapita EPL tena akitwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Championship? Sisi Yanga tuna uwezo wa wachezaji wakubwa kuliko wao na kama pesa na sisi tupo vizuri zaidi yao tuna Ghalib said Mohamed.

Hatuna cha kuhofia kuelekea mchezo huo na mashabiki wetu tunawaasa sana kufika uwanjani kifua mbele tena kwa kujiamini kwa sababu tuna malengo makubwa ya kufanikisha hilo,"Afisa Habari wa Yanga SC,Ali Kamwe.

Post a Comment

0 Comments