Waziri Balozi Mulamula ateta na Balozi Phee

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Nchi wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Balozi Molly Phee jijini New York.
Katika kikao hicho viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali kuhusiana na sekta ya afya zikiwemo jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa covid 19, kukomesha biashara haramu ya binadamu, mpango wa kuhuisha misaada kwa serikali na mpango wa kuhakikisha chakula kinapatikana.

Viongozi hao pia wamejadili changamoto nyingine zinazoikabili dunia kwa ujumla wake na namna ya kuweza kukabiliana nazo ikiwa ni pamoja na mpango wa MCC

Post a Comment

0 Comments