Waziri Simbachawene aongoza ujumbe muhimu SADC

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliolenga kuhusu namna ya kuchukua tahadhari za mapema katika hatua za Kudhibiti Majanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika picha akiwa katika Mkutano unaolenga namna ya kuchukua Tahadhari za Mapema katika hatua za Kudhibiti Majanga.

Mkutano huo wa siku mbili ulioanza Septemba 8 hadi 9, 2022 umedhaminiwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (UN World Meteorological Organization) na unafanyika mjini Maputo, Msumbiji .
Aidha, mkutano huo umetanguliwa na mkutano wa wataalamu wa masuala hayo ulioanza Septemba 5 hadi 7,2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news