Wizara ya Ardhi yatunukiwa Tuzo ya Heshima

NA MWANDISHI WETU

WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepata Cheti na Tuzo katika Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushika nafasi ya tatu kwa upande wa kundi la wizara.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti na Tuzo ya Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Ageline Mabula kwa wizara yake kushika nafasi ya tatu kwa upande wa kundi la wizara wakati wa kongamano hilo lililofanyika jijini Dodoma.

Tuzo hiyo imekabidhiwa Septemba 19, 2022 wakati wa Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi lililofanyika jijini Dodoma.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Dkt. Angeline Mabula na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Katika kongamano hilo Waziri Mkuu aliwataka wadau wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kuongeza nguvu katika kutoa huduma za uwezeshaji hasa maeneo ya pembezoni ya miji na vijijini ili kufikia malengo ya nchi katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri (Waliosimama nyuma) wakati wa Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika jijini Dodoma.

Aidha, aliitaka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuongeza kasi katika kupima na kurasimisha maeneo mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara (waliosimama nyuma) wakati wa Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika jijini Dodoma. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news