Wizara yasema hakuna samaki wanaohifadhiwa katika maji ya maiti

NA DIRAMAKINI

SERIKALI imesema hakuna mfanyabiashara wa samaki anayehifadhi samaki kwa kutumia maji ya kuoshea maiti kama ilivyodaiwa awali huko jijini Mwanza.

Aidha,Serikali imewatoa wananchi wasiwasi juu ya hofu ya kupata saratani kutokana na kutumia samaki waliohifadhiwa kwa njia hiyo.

“Jambo hili halina uhakika na watu wanahisia,” Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mheshimiwa Abdallah Hamis Ulega ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso (CHADEMA) kuwa Makamu wa Rais Dkt, Philip Mpango pia ameiagiza Wizara ya Afya kufanya utafiti ili kufahamu uhalisia na kuchukua hatua za kuzuia.

Mheshimiwa Pareso alidai kuwa, “siku za karibuni tumesikia taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa, uhifadhi wa samaki kwenve baadhi va maeneo hapa nchini unatumia dawa za kuhifadhia maiti jambo ambalo linaleta taharuki kwa wananchi na wananchi hawajui nini cha kufanya ili wasipate hao samaki waliohifadhiwa kwa namna hiyo;

Aidha,Mbunge huyo alihoji mkakati wa serikali wa kuhakikisha samaki hawahifadhiwi hivyo na kusababisha saratani kwa watanzania.

“Halipo jambo la namna hiyo kwamba samaki wanavuliwa Mwanza kuletwa Dodoma ama Dar es Salaam wahifadhiwe na maji ya maiti. Niwatoe wasiwasi wananchi kwamba wako salama,"amesema Mheshimiwa Ulega.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news