Alhaj Othman aungana na wananchi Kikwajuni kuadhimisha Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W)

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, usiku wa Oktoba 19,2022 amejumuika na waumini mbalimbali wa Kiislamu katika hafla ya Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Watu wa Kikwajuni na kufanyika katika viwanja vya Skuli ya Kisiwandui, Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja.
Alhaj Othman ambaye alikuwa ni mgeni rasmi wa hafla hiyo, ameungana pia na viongozi wa kitaifa wa Serikali, Dini, Jamii, Vyama vya Siasa na mamia ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya kisiwa cha Unguja.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watu wa Kikwajuni Sheikh Mohamed Suleiman Hibri na Katibu wa Jumuiya hiyo Sheikh Anas Omar Anas.

Post a Comment

0 Comments