Waziri Simbachawene:Vikao vya mashirikiano vitaendelea kufanyika

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imedhamiria kuendeleza kufanya Vikao vya Mashirikiano ili kufanya tafakari ya pamoja juu ya shughuli zinazofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene akizungumza katika Kikao cha Mashirikiano kilichofanyika jijini Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene katika mkutano wa kwanza wa Vikao vya Mashirikiano katika ngazi ya Mawaziri kilichofanyika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni jijini Zanzibar.

“Kushirikiana huku hakuepukiki na kwa bahati nzuri Serikali zote ni za Chama Cha Mapinduzi lazima tukutane mara kwa mara ili tuweze kutathimini ni namna gani tunatekeza Ilani ya Uchaguzi”.
Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakiwa katika kikao cha pamoja cha mashirikiano.

"Hii ni hatua nzuri tumefikia na ni lazima tuboreshe ratiba zaidi, ili tuende zaidi ya kiwango tunachokwenda sasa,"amesema Waziri.
Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakiwa katika kikao cha pamoja cha mashirikiano.

“Tusiishie kukutana ngazi hii tuu, tuweke utaratibu wa uratibu wa kukutanisha makundi na hasa vijana ili waweze kuufahamu Muungano wetu na wauenzi ili uwe na faida iliyokusudiwa na waasisi wetu wa nchi hizi mbili”.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma amesema, Muungano wetu ni wa kipekee na kuendelea kukutana hivi ni kuimarisha mawazo ya waasisi wetu wa Muungano.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Mhe.Hamza Hassan akizungumza katika Kikao cha Mashirikiano kilichofanyika jijini Zanzibar.

“Tunakaa tunazungumza mambo ya Wizara na taasisi zetu lakini tunakumbushana umuhimu wa Muungano na umoja wetu”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news