BUNDI WA GAMBOSHI SEHEMU YA 46

NA WILLIAM BOMBOM

Ilipoishia... Angalia mchungaji wa kanisa la WISDOM OF GOD na Amiri Othman Ally kwa sura ya nje walionekana kuwa watakatifu kumbe la hasha!.

Endelea

BUNDI WA GAMBOSHI alinishusha pale kambini kisha akaenda kwenye jengo lake maalumu la kupumzika.

Niliingia chumbani kwangu kisha nikajilaza kitandani huku nikiwa na mawazo kadha wa kadha. Nilijilaza kitandani huku macho yakiwa yameangalia darini nikiwaza na kuwazua juu ya vita iliyokuwa mbele yangu.

Kama kiongozi mkuu wa kambi ya kichawi hapo majengo nilipaswa kuibuka mshindi katika vita hivyo. Katika kuwaza na kuwazua hatimaye niliona njia pekee ya kuepusha vita hii ilikuwa ni kuwaua mahasimu wangu.

Uzembe wa aina yeyote kwa upande wangu ungepelekea maafa makubwa. Kambi ya Padri Jonasi Mzungu ilikuwa ni mwiba mkali kwa upande wangu, kambi hii ndiyo iliyohusika na mauaji ya viongozi wetu wakuu wa kambi.

Kambi hii ndiyo iliyohusika na kifo changu, maana mama na baba walijitoa kafara kwa kambi hii kama maagano ya kichawi yanavyoelekeza.

Mbaya zaidi kambi hii ilikuwa na maelewano na kambi ndogo ndogo nyingi za kichawi ukanda wa Nguruka, Mganza, Itebula na Mtegowanoti.

Hili pia lilikuwa ni mwiba kwa upande wa kambi yetu, hivyo basi katika kuwaza na kuwazua kitandani pale niliona ni vyema nisitishe ujenzi wa GAMBOSHI MPYA.

Lengo la kusitisha ujenzi huo ilikuwa ni kuwamaliza kwanza hasimu wetu ndipo tuendelee na ujenzi huo. Nikiwa kitandani hapo taratibu usingizi ilinichukua, nikapoteza kumbukumbu kwa mambo yote yaliyokuwa yakiendelea kwa wakati huo.

Nilikuja kushtuka muda saa sita mchana, nikapata chakula kisha nikaoga. Baada ya hapo niliwaita wasaidizi wangu kadhaa, wakaniletea taarifa za kambi za siku kisha nikazitumu kwa mkuu wetu kama ilivyo ada.

Baada ya hapo tulikaa kikao kifupi na viongozi hao, niliwasimulia kila kitu kilichotokea usiku wa leo baada ya kurudi toka Dodoma.

Hili kwa pamoja lilionekana kuwakera viongozi wenzangu, wengine walikumbuka tukio lisilo la kusahaulika lililofanywa na Padri huyo kwenye kambi yetu.

Tukio hilo lilikuwa ni la kuwaua viongozi wetu wakuu, hivyo muda wa kulipa kisasi ulikuwa umefika. Kwa pamoja tulikubaliana kumshikisha adabu usiku huo Padri huyo na kambi yake kwa ujumla.

Kikao kwa pamoja kilikubaliana kutenga siku hiyo kwa ajili ya kisasi, walipendekeza mchana huo kwenda kwa mchungaji wa kanisa la WISDOM OF GOD.

Mchungaji huyo alipaswa kushikishwa adabu ndani ya ministry yake, iliyokuwa karibu na eneo la majengo. Kikao kilikubaliana pia kufanya maandalizi ya kwenda usiku kambi ya Padri Jonasi Chambilacho.

Hayawi hayawi hatimaye yakawa, tuliondoka kambini kwetu mchana wa saa nane tukiwa wachawi kumi.

Tulijibadili maumbo tukachukua yale ya mbuzi, tukajigawa katika makundi mawili ya mbuzi watano. Tulikamata barabara itokayo CRDB Nguruka, tukanyoosha mpaka Lodge ya D Gube.

Njiani tulikuwa tukikutana na watu mbalimbali wakiwa kwenye shughuli zao. Pia tulikutana na wachawi mbalimbali wakiwa kwenye shughuli zao, walikuwa wamechukua maumbo ya wadudu mbalimbali wengine wakiwa kwenye maumbile yao ya kawaida.

Tulipofika Shelli ya Mwarabu tulipinda kushoto tukaiacha njia iendayo Bweru sokoni. Tukaifuata njia iendayo Mji wa Mganza, kabla ya kufika makaburini tulipinda kulia kuelekea kwenye Ministry hiyo ya WISDOM OF GOD.

Tuliambaa ambaa na ukuta wa ua wa jengo hilo, tukatokomea karibu na eneo la makaburi maana eneo la Ministry hiyo ilikuwa kubwa sana.

Tukachukua maumbo ya vipepeo tukazama ndani ya ua. Kundi la pili lilizunguka upande mwingine wa ua kisha likajibadili nyuki likaingia ndani ya ua.

Tulikutana ndani ya ua huo, kulikuwa na majengo mengi ila dawa zetu zikatuonesha jengo ambalo Mchungaji huyo hulitumia kuishi.

Ndani ya ministry hiyo kulikuwa na nyumba nyingi za wachungaji na watawa. Kwa haraka haraka ingekuchukua miaka dahali kujua undani wa mchungaji huyo.

Mbele yetu kulikuwa na jengo kubwa la kisasa, tuliingia ndani yake huku tukikagua chumba kimoja baada ya kingine.

Hakukuwa na jipya ndani ya vyumba hivyo, vitu vyote tulivyoviona vilikuwa vya kawaida sana. Mbaya zaidi hakukuwa na mtu hata mmoja, palikuwa kimya kiasi kwamba hata kama ungeangusha sindano ungeisikia.

Tukiwa kwenye harakati ya kumtafuta mchungaji huyo, ghafla tulikutana naye kwenye korido akitokea kwenye chumba fulani.

Kwa kuwa tulikuwa tumejipaka dawa ya kawaida za kutoonekana, ilimuwia rahisi kutuona. Kengele ya tahadhari ikaingia kichwani mwake, akaanza kukimbia kurudi kwenye chumba alichokuwa ametokea.

Tukamfuata hadi mlangoni hapo ambapo alikuwa amefunga kwa funguo kwa ndani. Tukaegemea ukutani tukatokeza chumbani humo tukitumia nguvu za madawa.

Mle chumbani hakukuwa na mtu yeyote, mbaya zaidi chumba hicho hakikuwa na makolokolo mengi. Kwa namna tulivyokuwa tumemkuta asingeweza kupotea kwa madawa, maana hakuwa amefanya maandalizi tulimshitukiza.

Kupotea kwa mchungaji huyo machoni kwetu hakuhusisha nguvu zozote za madawa, kwa namna moja au nyingine hapa lazima kuna njia ya ziada aliyokuwa ameitumia.

Katika zunguka zunguka yetu tulibaini kitufe fulani kilichokuwa ukutani, kitufe hicho kilikaa ukutani kama ua la kawaida.

Tulikivuta kitufe hicho ambacho kilikuwa kikivutia, ghafla upande wa sakafu ya chumba hicho ulijifungua.

Tayari majibu ya kitendawili chetu yakapatikana, tulisogea kwenye eneo hilo lililojifungua kisha tukazifuata ngazi zilizokuwa zikishuka chini. Kulikuwa na giza totoro chini ya jengo hilo tulimwaga dawa zetu pakawa peupe pe.

Ndugu msomaji chini ya jengo hilo kulikuwa na vyumba vingi zaidi ya vyumba vya jengo vinavyoonekana juu.

Tuliingia kwenye chumba cha kwanza kwa tahadhari kuu, lengo letu ilikuwa ni kumtia mikononi mwetu mchungaji huyo Mzungu.

Tulichokishuhudia chumbani humo hakikuwa kigeni machoni mwetu, kulikuwa kumejaa vichwa vya binadamu vilivyokaushwa.

Vilikaushwa na kubaki na ngozi yake ya asili, kila kichwa kilikuwa kimetolewa ubongo. Kwa kuwa tulikuwa tukijua kazi ya mchungaji huyu haikutupa tabu kuona mambo hayo, sisi wenyewe kazi yetu ilikuwa ni uchawi hivyo haikutushangaza.

Hapa niseme kidogo, kuna baadhi ya watu huingia nchini kwa kivuli cha dini kumbe siyo. Tazama mchungaji huyu alivyokuwa akiteketeza kizazi cha Waafrika kupitia mgongo wa dini.

Chumba kilikuwa kimejaa mafuvu ya binadamu, tulitoka kwenye chumba hicho tukaingia chumba kingine.

Chumba cha pili tulimutana na viungo vingine vya binadamu. Kulikuwa na nyeti za binadamu za kike na kiume.

Zipo zilizokuwa zimekaushwa zingine zikiwa mbichi, zipo zilizokuwa zikitiririka damu. Nadhani nyeti hizo alikuwa akizisafirisha kwenda nje.

Zilikuwa ni nyeti nyingi alizokuwa kazikata kutoka kwa binadamu, yawezekana ndiyo maana mission nyingi hujengwa karibu na makaburi.

Hii huwasaidia kufukua maiti usiku kisha kuchukua viungo vyao na kuvipeleka wanakokujua. Yawezakuwa kuna muda huwa wanaua raia kwa lengo la kupata viungo vyao, wengine hununua viungo hivyo au kubadilishana na wachawi wenzao kwa madawa.

Tulitoka kwenye chumba hicho tukaingia chumba cha tatu, mle tulikuta kuna viungo mbalimbali vya binadamu kama vile maini, bandama, filigisi na mioyo.

Viungo hivyo baadhi vilikuwa vimekaushwa huku vingine vikiwa vibichi kama tulivyoshuhudia chumba kilichopita. Hakuna muumini aliyekuwa akijua ujinga uliokuwa ukifanywa na mchungaji huyo.

Tulikwenda chumba cha nne tukabaini kilikuwa kimefungwa kwa ndani, tuliegemea kwenye ukuta tukayeyuka kisha tukaingia kwa ndani.

Alipotuona akayatoa macho mfano wa kibaka aliyekamatwa na jeshi la sungusungu. Nilimkata kofi moja akadondoka chini mithili ya gunia la mahindi.

Alijikuta akibwabwaja, " Please THE BOMBOM, don't kill Me" . ( Tafadhali THE BOMBOM usiniue). Nikamsindikiza kwa teke la tumbo akajikunja mfano wa tairi la bajaji.

Nilitema cheche kwa kiingereza kibovubovu " It's your time to kiss the ground, by any means you must die" ( Ni muda wako wa kuingia kaburini, kwa namna yeyote lazima ufe).

Nikamshindilia ngumi za mfululizo tumboni kwake huku akitapika, lengo langu ilikuwa ni kumuua kwa maumivu makali.

Alijikuny'ata pale chini kama mtoto mkiwa aliyefiwa na mamaye, tukamshika miguu yake kisha tukaanza kumburuza chini huku tukimpandisha juu.

Tulimvuta bila huruma huku akijigonga kwenye ngazi bila huruma, damu zilikuwa zikimtoka puani, mdomoni, masikioni pamoja na machoni.

Tulipomfikisha chumbani huko hatukutaka kufunga mlango wa kuingia vyumba vya chini. Tuliacha wazi tukiwa na lengo la kuwarahisishia upelelezi watakaokuja kuchunguza.

Tulichukua nyundo kisha tukaanza kumpiga kwenye goti mpaka tukalitengua, sauti ilikuwa imezuiwa kutoka njea. Tulimchapa akachapika, bahati nzuri wazungu huwa na ngozi laini hivyo damu zilimwagika na kutengeneza bwawa.

Mchawi mwenzangu alichukua upanga akaanza kumtenganisha mchungaji huyo kiungo kimoja baada ya kingine. Hatimaye tulimtenganisha mwili mzima, tukatoka ndani ya jumba hilo kisha tukarudi kambini kwetu. Hatukujali nini kingetokea kwenye lile kanisa, tulitaka ulimwengu mzima ujue kazi halisi ya mchungaji huyo.

Tulipofika kambini kwetu tuliendelea na maandalizi ya safari yetu, siku hiyo tulikuwa tumepanga kwenda kulipa kisasi kwenye kambi ya Padri Jonasi Chambilacho.

Bahati nzuri kambi hiyo nilikuwa nikiifahamu vyema maana nilikaa eneo hilo miaka kadhaa nikiwa msukule. Kambi hiyo ilikuwa ikitumiwa na wazazi wangu, yaani baba na mama baada ya kunitoa kafara nilipelekwa eneo hilo.

Siku zote nilitamani ifike siku ya kulipa kisasi kwa ujinga walionifanyia wazazi wangu pamoja na wachawi wenzao kina Padri Jonasi.

Tulitumia uwezo wa dawa zetu kugundua nguvu za kambi hiyo, kisha tukatengua nguvu hizo za uchawi wao. Tuliendelea na maandalizi mpaka ilipofika saa kumi na mbili jioni, niliwaita viongozi wachache kwa ajili ya kupanga mipango ya namna ya kuvamia kwenye kambi hiyo.

Ndugu msomaji unadhani THE BOMBOM na wafuasi wake watavamia kambi hiyo? Nini kitawatokea kwenye vita hiyo? Endelea kufuatilia kisa hiki cha kusisimua.

ZIMUHILA?
THE BOMBOM

Post a Comment

0 Comments