Dkt.Mwakyembe akabidhiwa jukumu madai kufeli wanafunzi LST

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt.Damas Ndumbaro ameunda timu ya wabobezi wa sheria saba watakaoongozwa na Dkt.Harrison Mwakyembe ambaye amewahi kuwa waziri kwenye wizara mbalimbali ili kuchunguza tatizo la kufeli kwa wanafunzi wa shule kuu ya sheria.

Waziri Dkt.Damas Ndumbaro ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la kufeli kwa wanafunzi katika taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) ambapo amesema jopo hilo la wataalamu litafanya kazi kwa siku 30 ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo.

Amewataja wajumbe wengine katika kamati hiyo ni Jaji Mstaafu Cililius Matupa aliyewahi kuwa mshauri wa rais Dk Jakaya Kikwete, Rashid Asaa ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma wa Zanzibar.

Wengine ni Gloria Kalabamu, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Alice Mtulo, Wakili mwandamizi kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mary Mniwasa, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dar Stock Exchange na John Kaombwe ambaye ni Mwanafunzi aliyehitimu LST.

”Kuundwa kwa tume hiyo kunakuja baada ya kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule Kuu ya Sheria Tanzania (LST) wakilalamika kurudia masomo kwa muda mrefu bila mafanikio,”amesema Dkt.Ndumbaro.

Waziri amesema kamati hiyo itakabidhiwa hadidu rejea na Kàtibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Makondo kesho Oktoba 13, 2022 na itafanya kazi kwa siku 30.

“Baada ya hapo, Mwenyekiti wake atakuja hadharani kutoa taarifa kwa waandishi kuhusu walichobaini lakini muamini kamati ina watu wenye weledi mkubwa sana,” amesema Dk Ndumbaro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news