Jaji Shindano la Urembo na Mitindo ya Viziwi Duniani awasili Dar

NA ADELADIUS MAKWEGA-WUSM

WAGENI kadhaa wanaotarajiwa kusimamia, kushiriki na kushuhudia Mashindano ya Utanashati, Urembo na Mitindo ya Viziwi Ulimwengu yanayofanyika Oktoba 29, 2022 Jijini Dar es Salaam wameanza kuwasili na huku wageni wengine zaidi wakitarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam hapo baadae.

Akizungumzia na vyombo vya habari Habibu Mrope, Rais wa Mashindano ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Afrika (MMDAF), mapema Oktoba 19, 2022 amesema kuwa mpaka sasa jaji Philippine Marsus akitokea Ubeligiji amewasili.

Huku ugeni mzito wa viongozi wakuu wa mashindano haya unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam hapo baadae. Rais huyo wa mashindano haya ya Afrika amewataja wageni hao wanasubiri kwa sasa,

“Bonita Leek ambaye ni Rais wa mashindano hayo duniani akitokea Marekani, Lorraine Darcy ambaye Katibu Mkuu wa mashindano kidunia akitokea Austaria na Jean Labess ambaye ni miongoni mwa majaji akitokea Ufaransa .”

Mwandishi wa habari hii ameshuhudia harakati za kuingia kwa wageni hao zikiendelea huku wakipokelewa na viongozi kadhaa wanaosimamia mashindano haya.
Huku ugeni huu ukitazamwa na wengi kama utasaidia kukuza utalii, kwani utalii si kutazama wanyama, kila pahala duniani kuna wanyama, utalii ni hata namna ya kumpokea mgeni tangu anavyoingia hadi siku anapoondoka nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments