Kalynda E-Commerce Ltd 'mikononi' mwa polisi

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi nchini limeanza kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko ya wananchi kutapeliwa fedha zao na kampuni ya Kalynda E-Commerce Ltd.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 15, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime.BRELA yafunguka sakata la Kalynda

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,Ofisi Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushiriana na taasisi nyingine za kiuchunguzi na za kifedha wameanza kuchunguza malalamiko hayo ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.

“Kutokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi kulalamika kutapeliwa fedha zao na kampuni waliyoeleza ni Kalynda E Commerce kwa njia ya mtandao, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushiriana na taasisi nyingine za kiuchunguzi na za kifedha wameanza kuchunguza.

“Jeshi la Polisi lingependa kutoa tahadhari tena kwa mara nyingine kwa Watanzania, kwani kama mtakumbuka tahadhari zilishawahi kutolewa kuanzia sakata la kampuni zingine ambazo ziliwahi kujinasibu kutoa huduma kama hizo,"imefafanua taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news