Malkia Maxima awasili Dar kwa ziara ya kikazi

NA MWANDISHI WETU

MALKIA wa Uholanzi, Malkia Maxima amewasili jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Kilimanjaro ambapo alianzia ziara yake jana tarehe 17 Oktoba 2022 baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 17 – 19 Oktoba, 2022.
Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima akipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya Malkia Maxima kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam, alipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza.
Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam. Pembeni yake mwenye suti ya kijivu ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza.

Malkia Maxima ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mfumo Jumuishi wa Fedha katika Maendeleo anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Oktoba 2022.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza akiteta jambo na Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima baada ya Malkia kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam.

Mbali na kukutana na Mhe. Rais Samia pia Malkia Maxima kabla ya kuhitimisha ziara yake hapa nchini, anatarajia pia kukutana na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.
Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news