MHE.OTHMAN AUNGANA NA WAUMINI WA KIISLAMU KUMUOMBEA DUA MAALIM SEIF

NA DIRAMAKINI

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, leo Oktoba 7, 2022 amejumuika na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, hapo Masjid Hanafi, Msikiti uliopo Mkunazini, Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja.
Ibada hiyo iliyowajumuisha Viongozi mbali mbali wa Dini, Siasa na Jamii, akiwemo Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo Zanzibar, Bw. Salim Bimani, imehusisha pia Dua Maalum ya Kumuombea Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, hadi alipofariki dunia, mnamo Februari 17, 2021.

Dua hiyo imeongozwa na Imamu Mkuu wa Masjid Hanafi, Sheikh Jamal Mukhtar.

Post a Comment

0 Comments