Mwanahabari afariki kwa kuangukiwa na kontena katika mkutano wa kisiasa

NA DIRAMAKINI

CHAMA cha Pakistan Movement for Justice (PTI) jana Oktoba 30, 2022 kimesitisha ziara ya muda mrefu baada ya mwanahabari wa kituo cha habari cha kibinafsi cha runinga, Sadaf Naeem kufariki kwa kuangukiwa na kotena la chama wakati akiripoti tukio karibu na Sadhoke.
PTI FILE PHOTO.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, Sadaf alikuwa akijaribu kupanda juu ya kontena kwa ajili ya kupata taswira nzuri wakati akiendelea kurusha matangazo ya moja kwa moja.

Hata hivyo, kwa sababu ya idadi kubwa ya washiriki waliokuwa wakishinikizwa kurudi nyuma katika tukio hilo ambalo liliongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho na Waziri Mkuu mstaafu Imran Khan kwa bahati mbaya, mwanahabari huyo alianguka chini kutoka kwenye kontena na gari likamkandamiza.

Kwa mujibu wa UrduPoint, Sadaf Naeem amezikwa jijini Lahore leo. Mwanahabari huyo alikuwa na umri wa miaka 35 na ameacha watoto watatu.
Dua ya maziko ya mwanahabari huyo ilifanyika jana usiku mara baada ya mwili wake kuhamishwa kutoka Kamoke na kupelekwa Hospitali ya Mayo.

Mwenyekiti wa PTI, Imran Khan alisitisha matembezi yake hayo ya muda mrefu alipojua kuhusu kifo cha mwanahabari huyo mwanamke.

Wakati huo huo Rais Arif Alvi, Waziri Mkuu Shehbaz Sharif na viongozi wengine wa kisiasa kutoka vyama tofauti pia walionesha huzuni na masikitiko juu ya kifo cha mwandishi huyo.

Waziri Mkuu ametangaza kutoa Rupia milioni 5 huku Serikali ya Punjab pia ikitangaza kutoa Rupia milioni 5 kwa familia ya mwandishi huyo.

Mapema leo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Rana Sanaullah ameiomba Serikali ya Punjab kufanya uchunguzi kuhusu tukio la kifo cha mwanahabari huyo wa kike wa kituo cha televisheni cha kibinafsi wakati wa matembezi marefu huko Sadhoke.

Katika taarifa yake, Waziri wa Mambo ya Ndani amesema, taarifa za waandishi wa habari za kufariki papo kwa papo zinatia shaka, hivyo tukio hilo na aliyemsukuma mwandishi wa habari huyo lazima akamatwe.

Waziri huyo wa Mambo ya Ndani amesema ikiwa Serikali ya Punjab haitashughulikia tukio hilo, basi Serikali ya Shirikisho itatimiza wajibu wake kwa haraka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news