NAIBU WAZIRI MAMBO YA NJE CZECH AWASILI NCHINI KWA ZIARA

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa amewasili nchi leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 2 hadi 4 Oktoba 2022.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa amewasili nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Tlapa amepokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme na Balozi wa Tanzania nchi Ujerumani ambaye pia anawakilisha Jamhuri ya Czech, Mhe. Dkt. Abdallah Possi.
Balozi wa Tanzania nchi Ujerumani ambaye pia anawakilisha Jamhuri ya Czech, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Akiwa nchini, Mhe. Tlapa kwa nyakati tofauti, atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Nchi-Tamisemi, Waziri wa Afya, Waziri wa Viwanda na Biashara, pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) pamoja na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Hospitali ya Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme.

Tanzania na Czech zimekuwa zikishirikiana katika sekta za elimu,utamaduni, afya, biashara na uwekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news