Rais Dkt.Mwinyi atoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Mussa Hassan Mussa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt,.Hussein Ali Mwinyi akitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Mussa Hassan Mussa, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar, alipofika nyumbani kwa familia ya marehemu Bwejuu Wilaya ya Kusini Unguja leo Oktoba 15, 2022.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na wanafamilia wa marehemu Mussa Hassan Mussa, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar, alipofika kijijini kwao marehemu Bwejuu kwa ajili ya kutoa mkono wa pole na kuhudhuria Kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika Msikiti wa Bwejuu Wilaya ya Kusini Unguja Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea marehemu Mussa Hassan Mussa, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar, kisomo hicho kilichofanyika katika Msikiti wa Bwejuu Wilaya ya Kusini Unguja leo na (kushoto kwa Rais) ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadidi Rashid na (kulia kwa Rais) ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Sheikh Khalid Ali Mfaume.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea marehemu Mussa Hassan Mussa, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar, kisomo hicho kilichofanyika katika Msikiti wa Bwejuu Wilaya ya Kusini Unguja leo na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadidi Rashid na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Mhe. Rajab Yussu Mkasaba (kulia kwa Rais), Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Sheikh Khalid Ali Mfaume.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj, Dkt.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na wanafamilia ya marehemu Mussa Hassan Mussa, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani wakiitikia dua ya kumuombea marehemu, alipofika kutoa mkono wa pole kwa familia kijijini kwao Bwejuu Wilaya ya Kusini Unguja leo, ikisomwa na Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume (kushoto kwa Rais).

Post a Comment

0 Comments