Rais Dkt.Mwinyi,Tshisekedi waangazia fursa

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi katika mazungumzo mafupi yaliofanyika Ikulu jijini Zanzibar, mwishoni mwa wiki iliopita.

Rais Tshisekedi aliyezuru nchini kwa ziara ya siku mbili kiserikali, kabla alipata fursa ya kufika Zanzibar kwa ziara binafsi na kuzungumza na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi.

Katika mazungumzo hayo Marais hao walijadili umuhimu wa kuangalia maeneo zaidi ya ushirikiano kati ya nchi mbili hizo kupitia sekta za kiuchumi na biashara, wakati huu biashara ya usafirishaji wa dagaa kutoka Zanzibar kwenda nchini Kongo ikishamiri.

Rais Dkt. Mwinyi alimuomba Rais Tshisekedi kuutangaza Utalii wa Zanzibar kwa wadau wa sekta ya Utalii nchini Kongo.

Aidha, Rais Tshisekedi alimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa mapokezi mazuri aliyopata yeye na ujumbe aliofuatana nao na akatumia fursa hiyo kuahidi kuongeza ushirikiano kati nchi mbili hizo kwa maslahi ya mataifa hayo na wananchi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news