Rais Felix Tshisekedi awasili Tanzania kwa ziara ya siku nne

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe. Felix Tshisekedi amewasili nchini Oktoba 21, 2022 kwa ziara ya kitaifa ya siku nne kuanzia tarehe 21 hadi Oktoba 25,2022.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe. Felix Tshisekedi akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe.Jamal Kassim Ali aliyempokea baada ya kuwasili nchini kupitia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kwa ziara ya kitaifa ya siku nne kuanzia tarehe 21 - 25, Oktoba 2022.

Mhe.Tshisekedi na Ujumbe wake amewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume jijini Zanzibar na kupokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe.Jamal Kassim Ali.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe. Felix Tshisekedi akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchni Kongo Mhe. Said Juma Mshana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar. 

Rais Tshisekedi akiwa Zanzibar anatarajia kukutana na mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi tarehe 22 Oktoba, 2022 na baadae atatembelea vivutio vya utalii.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe. Felix Tshisekedi akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Zanzibar, Bi. Mariam Haji Mrisho katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar. 

Tarehe 24 Oktoba 2022, Mhe.Tshisekedi anatarajia kuwasili jijini Dar es Salaam ambapo atapokelewa rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe. Felix Tshisekedi akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe. Jamal Kassim Ali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

Rais Tshisekedi anatarajia kuwa na mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan na baadaye atatembelea Bandari ya Dar es Salaam pamoja na mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).Mhe.Tshisekedi na ujumbe wake wanatarajiwa kuondoka nchini tarehe 25 Oktoba 2022.

Post a Comment

0 Comments