VIONGOZI WAMFUATA DOKTA SALMIN HUKO KIDOMBO

NA DIRAMAKINI

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman,Oktoba 21, 2022 amejumuika na Waumini wa Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, huko Mkwajuni Kidombo, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Baada ya ibada hiyo, iliyohudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dokta Hussein Ali Mwinyi, kumefanyika Hitma na Dua Maalum ya kuwaombea viongozi, Masheikh na Wazee waliopo hai na ambao wameshafariki dunia, ndani na nje ya kijiji hicho.
Harakati zote hizo ni sehemu ya Mwitikio wa Viongozi, kufuatia Mwaliko wa kila mwaka wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano ya Zanzibar, Alhaj Dokta Salmin Amour Juma, unaoambatana na Sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad (SAW), kiijijini hapo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini, Siasa na Jamii, wakiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi, wamehudhuria katika hafla hiyo.

Post a Comment

0 Comments