Serikali yatangaza viwango vipya vya tozo miamala ya simu, benki

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imetangaza viwango vipya vya tozo vya miamala simu na benki zikiwa zimepita siku chache tangu iahidi kuvipunguza kutokana na malalamiko ya wananchi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba, kupitia gazeti la Serikali la Septemba 30, mwaka huu amesema, mabadiliko hayo yamefanywa kupitia Sheria ya Mifumo ya Malipo (Sura ya 437) chini ya kifungu cha 46A(2).

Kwa mujibu wa jedwali la marekebisho hayo, kuhamisha shilingi 100 hadi shilingi 2,999 ni shilingi 10, kuhamisha shilingi 3,000 hadi shilingi 3,999 ni shilingi 14, shilingi 4,000 hadi shilingi 4,999 ni shilingi 27, kutuma shilingi 5,000 hadi shilingi 6,999 ni shilingi 54, kutuma shilingi 7,000 hadi shilingi 9,999 ni shilingi 56.

Aidha,vviwango vingine ni kutuma shilingi 10,000 hadi shilingi 14,999 ni shilingi 102, kutuma shilingi 15,000 hadi shilingi 19,999 ni shilingi 195, kutuma shilingi 20,000 hadi shilingi 29,999 ni shilingi 306, kutuma shilingi 30,000 hadi 39,999 ni shilingi 351.

Pia kutuma shilingi 40,000 hadi shilingi 49,999 ni shilingi 419, kutuma shilingi 50,000 hadi shilingi 99,999 ni shilingi 573, kutuma shilingi 100,000 hadi shilingi 199,999 ni shilingi 707, kutuma shilingi 200,000 hadi shilingi 299,999 ni shilingi 821.

Wakati huo huo,kutuma shilingi 300,000 hadi shilingi 399,999 ni shilingi 838, kutuma shilingi 400,000 hadi shilingi 499,999 ni shilingi 982, kutuma shilingi 500,000 hadi shilingi 599,999 ni shilingi 1,245, kutuma shilingi 600,000 hadi shilingi 699,999 ni shilingi 1,532.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shilingi 700,000 hadi ahilingi 799,999 ni shilingi 1,700, kutuma shilingi 800,000 hadi shilingi 899,999 ni shilingi 1,500, kutuma shilingi 900,000 hadi shilingi 1,000,000 ni shilingi 1,776, kutuma shilingi 1,000,001 hadi shilingi 3,000,000 ni shilingi 1,875, kutuma shilingi 3,000,001 na kuendelea ni shilingi 2,000.

Mbali na hayo, Kifungu cha 46A (2) kimeelezea kanuni za marekebisho ya kanuni za tozo ya miamala ya fedha ya kielektroniki za mwaka 2022 na zimeanza kutumika Oktoba 2,2022.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kanuni hizo zitajulikana kama kanuni za Marekebisho ya Kanuni za Tozo ya Miamala ya Fedha ya Kielektroniki za Mwaka 2022, na zitasomwa pamoja na Kanuni za Tozo ya Miamala ya Fedha ya Kielektroniki, 2022 ambazo hapa zitarejewa kama Kanuni Kuu.

Aidha, Kanuni Kuu zinarekebishwa katika kanuni ya 3 kwa kufuta tafsiri ya neno “kuhamisha fedha” na badala yake kuweka “kuhamisha fedha”ikimaanisha kuhamisha fedha kielektroniki kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji.

Wakati huo huo, tafsiri hiyo inaeleza kuwa, kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji huyo huyo.(Mwananchi)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news